Entertainment

Sakata la Hakimiliki Lavuruga Kazi Mpya ya Nandy na Jux

Sakata la Hakimiliki Lavuruga Kazi Mpya ya Nandy na Jux

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nandy, ameonyesha kuchukizwa na hatua ya msanii chipukizi anayefahamika kama Bride Vuitton, ambaye amewasilisha maombi YouTube kutaka wimbo wake mpya “Sweety” aliomshirikisha Jux kushushwa kwa madai ya hakimiliki {copyright}

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy ameeleza kuwa kufika hatua aliyo nayo sasa kumemgharimu jitihada na uwekezaji mkubwa, jambo ambalo anaona halithaminiwi na kitendo cha Bride Vuitton. Amesema kuwa msanii huyo mchanga ameona sakata hilo kama fursa ya kujitengenezea umaarufu, lakini hajafikiria hasara kubwa ambayo hatua hiyo inaweza kusababisha kwa kazi yake mpya.

Nandy ameongeza kuwa Bride Vuitton angetafuta njia nyingine za kujiweka kwenye tasnia bila kuhusisha kazi ya wasanii wenzake. Kwa mujibu wake, kitendo cha kutaka kushusha video ya “Sweety” siyo tu kumrudisha nyuma bali pia kinahatarisha ndoto na uwekezaji wake mzima.

Hata hivyo, licha ya kukasirishwa na kitendo hicho, Nandy amewataka mashabiki wake pia kumpa sapoti Bride Vuitton kwa kusikiliza wimbo wake “Joro”, akisisitiza kuwa njia bora ya kupata nafasi katika muziki ni kupitia jitihada na uvumilivu, si kwa kuua ndoto za wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *