Tech news

Samsung Yatoa Uhuru Mpya kwa Watumiaji Kupitia Quick Settings

Samsung Yatoa Uhuru Mpya kwa Watumiaji Kupitia Quick Settings

Kampuni ya teknolojia ya Samsung imeanza kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wake wa uendeshaji, ikilenga kutoa uhuru zaidi kwa watumiaji kupitia toleo jipya la One UI 8.5. Mabadiliko haya makuu yanahusu sehemu ya Quick Settings na Lock Screen, ambazo sasa zitakuwa completely customizable, hatua inayoashiria ushindani wa moja kwa moja na mfumo wa iOS wa Apple pamoja na ule wa Google Pixel.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Samsung, watumiaji wataweza kupangilia kila sehemu ya Quick Settings, kuchagua ukubwa wa vitufe, kuweka mpangilio wa sections wanavyotaka, na hata kubadilisha namna muonekano wa Lock Screen unavyoonekana. Hii ni mara ya kwanza kwa Samsung kuruhusu kiwango hiki cha uhuru katika muundo wa mfumo wake, hatua inayoonesha dhamira ya kampuni hiyo kuimarisha uzoefu wa mtumiaji.

Maboresho haya yanaifanya One UI 8.5 kuwa ya kipekee zaidi, huku ikitoa nafasi kwa watumiaji kuunda muonekano wa simu zao kwa mtindo wa kipekee kulingana na ladha na mahitaji yao. Samsung inalenga kuvutia zaidi wapenzi wa ubinafsishaji (customization) ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakivutiwa na uwezo wa Pixel n iPhone katika maeneo hayo.

Kwa sasa, mabadiliko haya yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi katika simu mpya zitakazokuja na One UI 8.5, kabla ya kusambazwa kwa masasisho kwenye baadhi ya vifaa vya zamani vya Samsung.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *