
Rais wa chama cha soka nchini Cameroon na mchezaji wa zamani wa Timu ya Inter Milan, Barcelona n.k Samuel Eto’o amshushia kichapo Mpiga picha Mjongeo (Videographer) baada ya kutoka kutazama mchezo wa Kombe la Dunia kati ya Brazil na Korea Kusini.
Baada ya kutoka Uwanjani Eto’o alionekana kupiga picha na mashabiki nje ya Uwanja wa 974 nchini Qatar na baadae alitokea Mtu aliyeshika kamera ambapo alionekama kuzungumza jambo na Eto’o.
Dakika Chache baadae Eto’o alionekana kushikwa na hasira na kuanza kumshambulisha jamaa huyo. Pamoja na kuzuiwa na watu Eto’o alifanikiwa kumpiga na kufanikiwa kumdondosha chini jamaa huyo.
Mpaka sasa haijafahamika ni sababu gani iliyopelelea Eto’o kumshushia kichapo jamaa huyo.