Entertainment

SARKODIE AFUNGUKA KUKUTANA NA BEYONCE

SARKODIE AFUNGUKA KUKUTANA NA BEYONCE

Rapa wa nchini Ghana Sarkodie amefunguka kuhusu tukio la kuwahi kukutana na Beyonce kwenye Tuzo za BET mwaka 2019. Sarkodie ambaye alishinda Tuzo ya Best International Flow usiku huo amefanya mahojiano na kuzungumzia tukio hilo ambalo wengi walishindwa kuamini.

Amesema “Kuna stori ya kuvutia ambayo iliwahi kunitokea, sikuwahi kupata uwezo wa kuizungumzia lakini Ice Prince alipokuja Ghana aliisimulia. Naamini mimi ningeisimulia hakuna yeyote ambaye angeniamini.” alieleza Sarkodie na kuendelea

“Nilikuwa nimekaa kwenye ukumbi wa Tuzo za BET na tulikuwa na Beyonce ambaye alikuwa pamoja na timu yake. Aliniona Mimi na akaja kusimama mbele yangu nilipokuwa nimekaa, kisha akainamisha kichwa chake chini (ishara ya kutoa heshima), kiukweli nilifikiri labda hajanifanyia mimi, nikageuka kutazama nyuma. Ice Prince akaniambia heshima hiyo Beyonce aliitoa kwangu. Kwa hiyo nilipoona anafanya kazi na wasanii wa Afrika kwenye album yake, nikasema kumbe hawa watu wanajua kinachoendelea kwenye muziki wetu” alimaliza Sarkodie.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *