
Msanii kutoka Uganda Sasha Brighton amefunguka kuwa hataki kusikia habari ya kuchumbiana kwani ameshaonja uchungu na utamu wake kwenye mahusiano yake ya zamani.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni mkali huyo wa ngoma ya “Byonjagadde”amesema kuwa sio kwamba haoni wanaume wa kuingia nae kwenye mahusiano bali hana hamu na mapenzi tena kwani wito wa kuoa umepotea moyoni mwake.
“Najua mimi ni mrembo sana na wanaume wananitamani lakini siko tayari kuingia kwenye mahusiano hivi karibuni. Watoto wangu ndio kipaumbele changu kwa sasa,” alisema.
Sasha brighton ana watoto wawili aliyopata na wanaume tofauti, ambao walimuumiza kimapenzi na kisha kumkimbia, wakimuachia majukumu ya malezi.