Entertainment

SAUTI SOL KUANZA ZIARA YA KIMUZIKI BARANI ULAYA MWEZI APRILI 2022

SAUTI SOL KUANZA ZIARA YA KIMUZIKI BARANI ULAYA MWEZI APRILI 2022

Kundi la muziki nchini Sauti Sol limetangaza ujio wa ziara yao ya kimuziki  Barani ulaya kwa kuanika mkeka wa mataifa ambayo watafanya shows.

Kupitia ukurasa wao rasmi wa instagram Sauti Sol, wameipa ziara hiyo jina la Sauti Sol  Europe Tour na itaanza Aprili Mosi, mwaka wa 2022 huko Barcelona nchini Uhispania na itafanyika ndani ya miji 19 kwa kipindi cha mwezi mmoja..

Ziara hiyo inatarajiwa kuzunguka kwenye miji mbalimbali nchini Ujerumani, Ureno, Ufaransa, Denmark, Uingereza, Belgium ambapo kilele chake kitakuwa nchini Uholanzi Juni 28 mwaka wa 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *