
Kundi la Sauti Sol limetangaza ujio wa Album hiyo ambayo kwa mujibu wao itaingiaa sokoni mwaka huu.
Kundi hilo ambalo lilichukua mapumziko kwenye muziki kwa muda wa miaka 2 wamethibitisha taarifa hiyo kupitia ukurasa wao wa.
“New year, New Album”, Waliandika
Hata hivyo hawajaweka wazi ni lini hasa Album hiyo itaingia sokoni wala wasanii ambao watasikika kwenye album hiyo.
Hii itakuwa ni album yao ya sita tangu waanze safari yao ya muziki miaka 17 iliyopita baada ya Midnight Train ya mwaka wa 2020.
Album zingine ni kama Sol Filosofia (2011), Mwanzo (2009), Afrikan Sauce (2019), na Live and Die in Afrika (2015).