Entertainment

SAUTI SOL WAAHIRISHA ZIARA YAO YA MUZIKI BARANI ULAYA

SAUTI SOL WAAHIRISHA ZIARA YAO YA MUZIKI BARANI ULAYA

Wasanii wa Kundi la Sauti Sol wametangaza kusitisha ziara yao ya muziki iliyopaswa kuanza rasmi mwezi huu wa Juni huko barani Ulaya.

Kupitia taarifa waliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii wasanii wa kundi hilo kwa masikitiko makubwa wamesema wamelazimika kupiga chini show hiyo kwa sababu ya changamoto ya kupata visa.

Sauti Sol Wamesema licha ya kutuma maombi ya kupata visa kwa ubalozi wa uingereza umewaambia wameshindwa kuwapatia visa kwa wakati kutokana mzozo unaoshuhudiwa kati ukraine na urusi.

Hata hivyo wamewaomba radhi  mashabiki wao wote ambao kwa njia moja au nyingine wameathirika na uamuzi wao huo huku wakiahidi kufanya mazungumzo na mapromota wa muziki nchini uingereza kutoa tarehe nyingine ya kufanyika kwa ziara yao ya muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *