
Kundi la Sauti Sol limetangaza rasmi tarehe ambayo watalifanya tamasha la muziki liitwalo ‘Sol Fest’.
Kulingana na sauti sol, tamasha lao la siku mbili limepangwa kufanyika Desemba 11 na 12 mwaka huu wa, 2021.
Akizungumzia kuhusu mustakabali wa kundi la Sauti Sol baaada ya wasanii wake kuzindua utaratibu wa kuachia kazi zao kama wasanii wa kujitegemea, bien ambaye ni member wa Sauti Sol amesema kundi hilo lipo mbioni kuachia album yao mpya mwakani ambayo tayari imekamilika.
Sauti sol wameweka wazi hilo baada ya kuzindua programu yao ya simu iitwayo ‘Hustle Sasa’ inayolenga kuwaunganisha watengeneza maudhui na mashabiki wao huku wakiingiza pesa kupitia kazi zao.