Entertainment

Sean Kingston Ahukumiwa Miaka 3.5 Gerezani kwa Ulaghai

Sean Kingston Ahukumiwa Miaka 3.5 Gerezani kwa Ulaghai

Mwanamuziki maarufu Sean Kingston amepewa kifungo cha miaka mitatu na nusu gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki katika mpango mkubwa wa utapeli wa zaidi ya dola milioni 1 nchini Marekani.

Kingston pamoja na mama yake, Janice Eleanor Turner, wanadaiwa kutumia umaarufu wa Kingston na akaunti zake za mitandao ya kijamii kuwahadaa wafanyabiashara wa bidhaa za kifahari, wakiwahakikishia malipo ambayo hayakufanyika.

Badala ya kutimiza ahadi za malipo, walitumia stakabadhi za uhamisho wa fedha za kughushi kama ushahidi wa manunuzi.

Hukumu hiyo imetolewa jana Ijumaa katika Mahakama ya Shirikisho iliyoko Florida Kusini. Sean Kingston alipatikana na hatia ya makosa manne ya ulaghai kupitia njia ya mawasiliano (Wire Fraud) pamoja na kosa moja la kula njama ya kutenda ulaghai huo.

Mwezi uliopita, mama yake, Janice Eleanor Turner, alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela pamoja na miaka mitatu ya kusimamiwa chini ya uangalizi wa karibu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *