
Wawakilishi wa Afrika kwenye michuano ya Kombe la Dunia timu ya Taifa ya Senegal imeondoshwa kwenye hatua ya 16 bora ya mashindano hayo baada ya kupokea kichapo kizito cha 3-0 kutoka kwa England
Jordan Henderson na Harry Kane waliifungia England katika kipindi cha kwanza huku bao la tatu likifungwa na Bukayo Saka mwanzoni mwa kipindi cha pili.
Kocha wa Senegal Aliou Cisse anasema walipata nafasi lakini walishindwa kuzitumia hasa baada ya katikati ya kipindi cha kwanza, Krépin Diatta aliingilia pasi mbaya kutoka kwa Harry Maguire na krosi yake ikasababisha hati hati kwenye lango la Uingereza. Ismaila Sarr alipiga krosi ya ikagongwa mwamba wa Jordan Pickford na kutoka nje.
Wakati huo huo Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia timu ya Taifa ya Ufaransa imefanikiwa kutinga hatua ya robo ya fainali baada ya kuizaba Poland 3-1 katika mchezo wa 16 Bora
Kylian Mbape alifunga mara mbili na kutoa pasi moja ya mwisho kwa Olivier Giroud aliyeweka rekodi ya kuwa mfungaji Bora wa muda wote kwenye kikosi cha Ufaransa kwa kufikisha mabao 52
Ufaransa sasa atakutana na England kwenye hatua ya robo fainali