
Kwa muda sasa, kumekuwa na majabizano makali kati ya sosholaiti maarufu nchini Uganda Sipapa na mpenzi wake wa zamani Serena Bata. Sipapa amekuwa akimshutumu vikali Serena Bata kwa kutunga nyimbo zilizomlenga moja kwa moja.
Kwenye mahojiano yake wiki kadhaa zilizopita, Sipapa alisikika akimuonya serena bata akome kumtaja kwenye nyimbo zake ambapo alienda mbali na kutishia kugoma kumpa msaada wa kifedha ambao anadai amekuwa akimpa.
Sasa katika mahojiano mapya, msanii Serena Bata ameibuka na kukanusha madai ya kurudiana na Sipapa, kwa kusema kwamba hawawezi fanya tena kazi na meneja wake huyo wa zamani.
Hitmaker huyo wa βBinumaβ amedai kwamba sio kila wimbo anaoimba unamlenga sipapa kwani amekuwa akitoa muziki kwa ajili ya mashabiki zake.
Hata hivyo Serena Bata amesema juhudi za sipapa kumshawishi waanzisha mahusiano mpya ya kimapenzi hazitafanikiwa kwani amemsahau kabisa kwenye maisha yake.