Gossip

Shangazi wa Flaqo Afunguka Baada ya Kuzuiwa Mitandaoni

Shangazi wa Flaqo Afunguka Baada ya Kuzuiwa Mitandaoni

Shangazi wa mchekeshaji maarufu Flaqo, anayejulikana kama Nyakwar, ameifunguka kwa uchungu baada ya kudaiwa kuzuiwa na msanii huyo kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia TikTok Live, Nyakwar amesema kitendo hicho hakijamuumiza kwa kuwa hajawahi kumtegemea Flaqo wala kupata msaada wake katika maisha yake. Amefafanua kuwa angeumia zaidi endapo angezuiwa na watu wa nje, ambao amesema mara nyingi wamekuwa msaada kwake, kuliko watu wa familia.

Kwa mujibu wa Mwanamama huyo, familia yake hawajawahi kushiriki katika maendeleo yake, hivyo haoni jambo la kushangazwa kwa maamuzi ya mchekeshaji huyo kumuondoa kabisa kwenye mitandao yake ya kijamii.

Kauli yake inakuja siku chache mara baada kudai kwamba Flaqo amekuwa akimtelekeza mama yake mzazi na hajawahi kumpa msaada wowote licha ya kuwa na uwezo mkubwa kiuchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *