Entertainment

Sheebah Karungi atangaza kuzindua App ya filamu

Sheebah Karungi atangaza kuzindua App ya filamu

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Sheebah Karungi ameweka wazi mpango wake wa kuingia kwenye baishara ya filamu.

Kwenye mkao na wanahabari sheebah amesema safari hii hatoigiza bali yupo mbioni kuzindua programu yake ya simu ambayo itawapa watumiaji wa mitandaoni ya kijamii fursa ya kutizama filamu za nchini kwao uganda wakiwa maeneo mbali mbali duniani.

Hitmaker huyo wa Kanselawo amesema amechukua hatua hiyo ya kuwekeza kwenye biashara ya Filamu kutengeneza ajira kwa vijana wengi nchini uganda ambapo amejinasibu kuwa ana mpango wa kutoa ajira kwa zaidi ya watu 60.

Hiii Itakuwa ni biashara ya nne kwa sheebah Karungi kuwekeza kando na muziki ikizingatiwa kuwa ana miliki ukumbi wa uburudani uitwao Red terrace Bar, kampuni ya taulo za kike iitwayo Sheebah Holic pads na kampuni ya Red Events inayojishughulisha masuala ya kuandaa sherehe za harusi na nyingine nyingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *