
Staa wa muziki nchini Uganda Sheebah Karungi ameripotiwa kuwa yupo mbioni kuja na lebo yake ya muziki.
Kulingana na chanzo cha karibu na msanii huyo sheebah ana mpango wa kuanzisha na lebo ya muziki ambayo itawasajili wasanii wa kike.
Chanzo hicho kimeenda mbali zaidi na kusema kuwa kuanzisha lebo hiyo ilikuwa moja kati ya ndoto ya sheebah Karungi kukukuza vipaji vya watoto wa kike nchini Uganda.
Hata hivyo juhudi za vyombo vya habari nchini Uganda kumtafuta Sheebah athibitishe suala hilo halikuzaa matunda ila tutakufahamisha katika taarifa zetu za baadae kama mrembo huyo anakuja na lebo au la.
Utakumbuka Sheebah na aliyekuwa meneja wake Jeff Kiwa waliingia ugomvi mbaya mwishoni mwa mwaka wa 2021 jambo lilompelekea mrembo huyo kuvunja mkataba wake na lebo ya Team No Sleep na kuanza kufanya muziki kama msanii wa kujitegemea.