
Baada ya interview ya Ali Kiba kutrend akizungumzia sakata la kutomualika msanii mwenzake shilole katika uzinduzi wa album yake ya Only One King ,tayari mrembo huyo ameweza kumjibu Ali Kiba kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Katika maelezo yake Shilole ameonekana kutoridhishwa na kauli ya ali kiba kuwa hakumualika kwenye listening party ya album yake na kudai kuwa yeye hakwenda katika shughuli ile kama mvamizi.
Haikushi hapo ameenda mbali na kueleza kuwa Ali Kiba amethibitisha kwa walimwengu kuwa ana kiburi cha ushamba, kuvimba na kupandisha mabega katika namna isiyo stahili.
Sekeseke hili limetokea baada ya mjasiriamali Esha Buheti kulalamika kuwa hapewi thamani na Ali kiba licha ya kumuunga mkono kwenye muziki wake kwa asilimia kubwa.
Kauli hiyo ya Esha inadaiwa kutolewa baada ya Shilole ambaye hajawahi kuwa shabiki wa Ali kiba kualikwa kupitia ukurasa rasmi wa Alikiba huku Esha akialikwa kupitia ukurasa wa Instagram wa Kings Music.