Entertainment

Shilole Ashukuru Upendo wa Mashabiki Licha ya Polisi Kutilia Shaka Taarifa za Ajali Yake

Shilole Ashukuru Upendo wa Mashabiki Licha ya Polisi Kutilia Shaka Taarifa za Ajali Yake

Msanii wa Bongo Flava na mjasiriamali, Shilole, ameendelea kupokea upendo mkubwa kutoka kwa mashabiki na Watanzania kwa ujumla, baada ya kudai kunusurika katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia Januari 3 katika eneo la Malagarasi, mkoani Kigoma.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Shilole ametoa shukrani kwa watu wote waliomtumia jumbe za pole na za kutia moyo, wakiwemo ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki, akieleza kuwa upendo na dua zao zimekuwa chanzo kikubwa cha faraja na nguvu kwake.

Mwanamama huyo, ameongeza kuwa kila pumzi anayovuta ni ushuhuda wa uhai wake, huku akitoa sifa na utukufu kwa Mungu.

Hata hivyo, wakati mashabiki wakionyesha mshikamano, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limeendelea kutilia shaka taarifa za ajali hiyo, likisema kuwa halikupokea taarifa rasmi zinazothibitisha tukio hilo. Polisi wamemtaka mhusika kuwasilisha taarifa sahihi kwa mamlaka husika ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *