Gossip

Huddah Aumizwa na Kitendo cha Shabiki Kumlinganisha na Vera Sidika

Huddah Aumizwa na Kitendo cha Shabiki Kumlinganisha na Vera Sidika

Socialite kutoka Kenya Huddah Monroe ameweka wazi kuwa hatavumilia tena kashfa au kejeli mwaka 2026, baada ya shabiki mmoja mitandaoni kudai kuwa mpinzani wake Vera Sidika alimzidi kimafanikio mwaka 2025.

Akimjibu shabiki kwa hasira, Huddah ameeleza kuwa kitendo cha kulinganishwa na mafanikio ya watu wengine kimekuwa kikimuumiza kihisia, akisema watu wengi hawajui juhudi, changamoto na safari aliyopitia kufikia alipo leo.

Mrembo huyo, amesema kuwa heshima yake ni jambo la msingi na kwamba yeyote atakayemvunjia heshima atamchukulia hatua kali za kisheria.

Huddah, ameeleza kuwa amechukua uamuzi huo ili kulinda afya yake ya akili na pia iwe funzo kwa wale wanaotumia mitandao ya kijamii kumshambulia au kumkejeli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *