
Mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Shorn Arwa, ametoa somo kwa wanawake kuhusu maadili na kujithamini, akiwaasa kujitafutia fedha badala ya kutegemea wanaume kwa msaada wa kifedha.
Kupitia mitandao ya kijamii, Arwa ameeleza masikitiko yake kufuatia matukio aliyoshuhudia katika tamasha la Luo Festival, akisema baadhi ya tabia zilizojitokeza ni za aibu na zinapaswa kukemewa.
Arwa amedai kuwa baadhi ya warembo walijidhalilisha kwa kufanya vitendo vya aibu hadharani ili kupata tiketi za kuingia kwenye tamasha hilo. Ameeleza kuwa wanawake wengi walijikuta wakifanya mapenzi na wanaume kwenye nyasi ili kupata tiketi, hali ambayo ametaja kuwa ya kusikitisha.
Mrembo huyo amesisitiza kuwa kila mwanamke ana haki na uwezo wa kufanikisha maisha yake bila kulazimika kupitia njia za kudhalilisha utu wake. Pia amehimiza umuhimu wa wanawake kujitafutia kipato na kuepuka utegemezi wa kupita kiasi kwa wanaume, akiongeza kuwa mustakabali wa wanawake ni wenye matumaini makubwa.
Ujumbe huo wa Shorn Arwa umeibua mjadala mitandaoni, wengi wakimuunga mkono kwa kuhimiza wanawake kujitegemea na kulinda heshima zao, huku wengine wakisisitiza umuhimu wa elimu ya kujikimu kimaisha kwa vijana.