Shorn Arwa Ajizawadia Toyota Harrier Mpya Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa

Shorn Arwa Ajizawadia Toyota Harrier Mpya Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa

Influencer wa Kenya, Shorn Arwa, amejizawadia gari jipya aina ya Toyota Harrier lenye vifaa kamili kwenye siku yake ya kuzaliwa, hatua iliyozua pongezi na gumzo mitandaoni. Kupitia chapisho lake la kusherehekea birthday yake, Shorn Arwa ameonyesha shukrani kubwa kwa Mungu na kujivunia hatua aliyofikia, akieleza kuwa mambo aliyokuwa akiyaomba hapo awali sasa yamekuwa sehemu ya maisha yake ya kila siku. Katika ujumbe wake, amesema kuwa kujinunulia gari hilo ni ushahidi wa kazi, nidhamu na kujitokeza kila siku kwa ajili ya ndoto zake. Mrembo huyo, amefafanua kuwa Toyota Harrier hiyo mpya imenunuliwa kwa jina lake halali la kiserikali, jambo alilosisitiza kwa furaha akieleza kuwa ni SUV yenye vifaa vyote vya kisasa. Shorn Arwa pia amejipongeza kwa juhudi na uthubutu wa kuendelea kusukuma mbele licha ya changamoto, akihitimisha ujumbe wake kwa kujitakia heri ya siku ya kuzaliwa kwa maneno yaliyojaa upendo na matumaini makubwa ya mafanikio zaidi.

Read More
 Shorn Arwa Awapa Somo Wanawake Wanaopost Picha Baada ya Kuvunja Mahusiano

Shorn Arwa Awapa Somo Wanawake Wanaopost Picha Baada ya Kuvunja Mahusiano

Mshawishi wa mitandaoni kutoka Kenya, Shorn Arwa, ametoa somo kwa wanawake kuacha tabia ya kupakia picha nyingi mtandaoni pindi mahusiano yao ya kimapenzi yanapovunjika. Kupitia Insta Story yake, amesema wanawake wengi mara baada ya kuachwa huingia katika harakati za kuonesha maisha ya kifahari, kupendeza na kujiamini kupitia mitandao ya kijamii ili kuthibitisha kuwa bado wako imara. Hata hivyo, Arwa anaona tabia hiyo kama ushamba na jaribio la kutafuta uthibitisho kutoka kwa watu wengine badala ya kujijengea heshima na kuponya nafsi zao. Kwa mtazamo wake, badala ya kutumia mitandao ya kijamii kuthibitisha hali zao, wanawake wanapaswa kuelekeza nguvu katika kujitunza na kujijenga kifedha. Kulingana naye, kuporomoka kwa uhusiano si mwisho wa maisha, bali ni nafasi ya kujifunza na kukua.

Read More
 Shorn Arwa Awashambulia Mastaa wa Kenya Wanaodai Hawataki Umaarufu

Shorn Arwa Awashambulia Mastaa wa Kenya Wanaodai Hawataki Umaarufu

Mtayarishaji wa maudhui mtandaoni, Shorn Arwa, amewakemea mastaa wanaodai kwamba wanachukia maisha ya umaarufu ilhali wao wenyewe huendelea kuchapisha maisha yao kwenye mitandao ya kijamii kila wakati. Kupitia instastory yake, Arwa amesema ni unafiki kwa mtu kulalamika kuhusu shinikizo la umaarufu lakini bado akawa wa kwanza kushiriki kila tukio la maisha yake hadharani. Mrembo huyo ameongeza kuwa mtu anayehisi kero na maisha ya umaarufu ana uwezo wa kuishi maisha ya kawaida bila kulazimika kutangaza kila hatua kwa mashabiki. Kauli ya Arwa imeibua maoni mseto miongoni mwa mashabiki na wanamitandao, baadhi wakikubaliana naye kwamba mastaa hawawezi kukwepa umaarufu endapo wao wenyewe ndio wanauendeleza. Wengine hata hivyo wameeleza kuwa ni jambo la kawaida kwa mtu kuhisi kuchoshwa na presha za macho ya umma hata kama anapenda kushirikisha mashabiki wake.

Read More
 Shorn Arwa Awapa Somo Mabinti Baada ya Tukio la Aibu Luo Festival

Shorn Arwa Awapa Somo Mabinti Baada ya Tukio la Aibu Luo Festival

Mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Shorn Arwa, ametoa somo kwa wanawake kuhusu maadili na kujithamini, akiwaasa kujitafutia fedha badala ya kutegemea wanaume kwa msaada wa kifedha. Kupitia mitandao ya kijamii, Arwa ameeleza masikitiko yake kufuatia matukio aliyoshuhudia katika tamasha la Luo Festival, akisema baadhi ya tabia zilizojitokeza ni za aibu na zinapaswa kukemewa. Arwa amedai kuwa baadhi ya warembo walijidhalilisha kwa kufanya vitendo vya aibu hadharani ili kupata tiketi za kuingia kwenye tamasha hilo. Ameeleza kuwa wanawake wengi walijikuta wakifanya mapenzi na wanaume kwenye nyasi ili kupata tiketi, hali ambayo ametaja kuwa ya kusikitisha. Mrembo huyo amesisitiza kuwa kila mwanamke ana haki na uwezo wa kufanikisha maisha yake bila kulazimika kupitia njia za kudhalilisha utu wake. Pia amehimiza umuhimu wa wanawake kujitafutia kipato na kuepuka utegemezi wa kupita kiasi kwa wanaume, akiongeza kuwa mustakabali wa wanawake ni wenye matumaini makubwa. Ujumbe huo wa Shorn Arwa umeibua mjadala mitandaoni, wengi wakimuunga mkono kwa kuhimiza wanawake kujitegemea na kulinda heshima zao, huku wengine wakisisitiza umuhimu wa elimu ya kujikimu kimaisha kwa vijana.

Read More