Mshawishi wa mitandaoni kutoka Kenya, Shorn Arwa, ametoa somo kwa wanawake kuacha tabia ya kupakia picha nyingi mtandaoni pindi mahusiano yao ya kimapenzi yanapovunjika.
Kupitia Insta Story yake, amesema wanawake wengi mara baada ya kuachwa huingia katika harakati za kuonesha maisha ya kifahari, kupendeza na kujiamini kupitia mitandao ya kijamii ili kuthibitisha kuwa bado wako imara.
Hata hivyo, Arwa anaona tabia hiyo kama ushamba na jaribio la kutafuta uthibitisho kutoka kwa watu wengine badala ya kujijengea heshima na kuponya nafsi zao.
Kwa mtazamo wake, badala ya kutumia mitandao ya kijamii kuthibitisha hali zao, wanawake wanapaswa kuelekeza nguvu katika kujitunza na kujijenga kifedha. Kulingana naye, kuporomoka kwa uhusiano si mwisho wa maisha, bali ni nafasi ya kujifunza na kukua.