LifeStyle

Shorn Arwa Awashambulia Mastaa wa Kenya Wanaodai Hawataki Umaarufu

Shorn Arwa Awashambulia Mastaa wa Kenya Wanaodai Hawataki Umaarufu

Mtayarishaji wa maudhui mtandaoni, Shorn Arwa, amewakemea mastaa wanaodai kwamba wanachukia maisha ya umaarufu ilhali wao wenyewe huendelea kuchapisha maisha yao kwenye mitandao ya kijamii kila wakati.

Kupitia instastory yake, Arwa amesema ni unafiki kwa mtu kulalamika kuhusu shinikizo la umaarufu lakini bado akawa wa kwanza kushiriki kila tukio la maisha yake hadharani.

Mrembo huyo ameongeza kuwa mtu anayehisi kero na maisha ya umaarufu ana uwezo wa kuishi maisha ya kawaida bila kulazimika kutangaza kila hatua kwa mashabiki.

Kauli ya Arwa imeibua maoni mseto miongoni mwa mashabiki na wanamitandao, baadhi wakikubaliana naye kwamba mastaa hawawezi kukwepa umaarufu endapo wao wenyewe ndio wanauendeleza.

Wengine hata hivyo wameeleza kuwa ni jambo la kawaida kwa mtu kuhisi kuchoshwa na presha za macho ya umma hata kama anapenda kushirikisha mashabiki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *