
Msanii wa Bongofleva kutoka Konde Music Worldwide, Harmonize amesema hajawai kutuma watu kuzungumza vibaya kuhusu washindani wake.
Hitmaker huyo wa “Teacher” amefunguka hayo kwenye kituo kimoja cha radio ambapo ameeleza kuwa haweza kumtuma mtu yeyote kuwashambulia mahasidi wake kwa sababu hakuna kitu chochote wataongeza kwa kazi zake.
“Mkiona mtu yeyote anaenda kumzungumzia mtu fulani basi ujue ni maamuzi yake na mimi binafsi siwezi kumtuma mtu yeyote kwa sababu hanisaidii.” alisema Harmonize.
Ikumbukwe Harmonize ambaye alifunga mwaka kwa kuachia albamu yake ya pili, High School, hadi sasa lebo yake ina wasanii kama Ibraah, Killy, Cheed, Angella na Young Skales toka Nigeria.