Entertainment

Sina mpango wa kumuoa Prima Kardash – Geosteady

Sina mpango wa kumuoa Prima Kardash – Geosteady

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Geosteady ameamua kutoa ya moyoni kuhusu hatma ya uhusiano wake na mzazi mwenzie Prima Kardash.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema hana mpango wa kufunga ndoa hivi karibuni na Baby Mama wake huyo.

Kulingana na Hitmaker huyo wa “Sembera”, alipoteza hamu ya kuwa kwenye ndoa na Kardash kutokana kujihusisha na vitendo vya usaliti.

“Sioni nikimuoa Prima, nilikuwa na maono hayo hapo nyuma lakini sina tena,” Geosteady alifichua.

Geosteady na Prima ambao walifufua penzi lao miezi kadhaa iliyopita kwa pamoja wana watoto wawili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *