Others

SIZE 8 AWAJIBU KITAALAM WANAOMKOSOA MTANDAONI

SIZE 8 AWAJIBU KITAALAM WANAOMKOSOA MTANDAONI

Msanii wa Nyimbo za Injili nchini Size 8 amewajibu kisomi waliomkosoa baada ya video kusambaa mtandaoni ikimuonyesha akitoa mapepo  kutoka kwa waumini wa kanisa moja jijini Nairobi.

Katika mahojiano yake na Presenter Ali, Size 8 amesema hana muda wa kuwaaminisha watu kazi anayomfanyia mungu kwani kuna kipindi watakuja kuamini harakati zake za kusambaza injili.

Size 8 ambaye ni kasisi amesema watu wanaomkejeli mtandaoni hawatamkatisha tamaa ya kumtumikia mungu kwa kuwa baadhi yao shetani anawatumia kusambaratisha injili.

Hitmaker huyo wa “Mateke” amesema hayo alipolamba dili nono ya kuwa balozi wa bidhaa za urembo za RD Beauty.

Ikumbukwe tangu Size 8 aachane na muziki wa kidunia mwaka wa 2013 na kuhamia kwenye muziki wa injili watu wamekuwa wakikosoa kwa kwenda kinyume na maandiko matakatifu ya kikristo kutoka mienendo yake ya kimaisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *