Entertainment

Size 8: Nilitoka Mazingira ya Kishetani Kabla ya Kuokoka

Size 8: Nilitoka Mazingira ya Kishetani Kabla ya Kuokoka

Msanii wa injili kutoka Kenya, Size 8, amefunguka kuhusu maisha yake ya awali akisema alitoka kwenye mazingira ya kishetani.

Akipiga stori na podcast ya Mwakideu Live, amesema anaamini kuwa hali hiyo ndiyo iliyochangia kwa kiasi kikubwa kupaa kwake kwa kasi kwenye muziki wa secular na kupata umaarufu mkubwa katika kipindi kifupi.

Size 8 ambaye pia ni kasisi, ameeleza kwamba ingawa alipata nafasi na mafanikio ya haraka katika tasnia ya burudani, hakuwahi kufurahia amani ya kweli moyoni mwake. Kwa mtazamo wake, nguvu alizokuwa akizipata zilikuwa za giza na ndizo zilizomsukuma mbele kwa njia isiyo ya kawaida.

Baada ya kuokoka na kugeukia muziki wa injili, Size 8 sasa anasema hadithi yake ni ushuhuda wa jinsi Mungu anavyoweza kubadilisha maisha ya mtu yeyote. Anatumia mfano wake kuwatia moyo watu wanaopitia changamoto kuamini kwamba mabadiliko ni kitu cha kweli na kinachowezekana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *