
Mara baada ya Rapa Young Lunya kutoka nchini Tanzania kusaini kuwa chini ya Sony Music Africa, lebo hiyo ya kimataifa imeweka wazi kolabo kubwa za Rapa huyo zinazotarajiwa kutoka siku za mbeleni.
Katika taarifa yao kwa umma, Sony Music wamesema kuna ngoma za Lunya zinazokuja alizoshirikiana na Khaligraph Jones, Shomadjozi na Diamond Platnumz.
Katika hatua nyingine, Sony Music wametangaza kuwa Juni 10, mwaka wa 2022 Young Lunya ataachia wimbo wake mpya, uitwao Vitu Vingi ambao utakuwa wa kwanza chini ya lebo hiyo.
Utakumbuka Sony Music Africa imewahi kufanya kazi na wasanii wa Tanzania kama Rose Muhando, Alikiba na wengine wengi.