
Staa wa muziki kutoka nchini Spice Diana Uganda ameachia rasmi EP yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.
EP hiyo inakwenda kwa jina la Star Gal ina jumla ya nyimbo 4 za moto ikiwa na kolabo mbili kutoka kwa wakali kama Jose Chameleone, John Blaq na Daddy Andre.
Star Gal ambayo kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani ina ngoma kama Boss,Bwotyo,Sankalebwa na Toli Weka.
Hii ni EP ya kwanza kwa mtu mzima Spice Diana tangu aanze safari yake ya muziki na mwaka wa 2015.