
Nyota wa muziki kutoka Uganda Spice Diana ametangaza kuja na Extended Playlist ‘EP’ yake aliyoipa jina la ‘Stargal.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Spice Diana amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kuipokea EP yake hiyo ambayo kwa mujibu wake itaingia sokoni hivi karibuni.
Pamoja na kutangaza ujio wa ep hajaweka wazi idadi nyimbo na wasanii aliowashirikisha kwenye EP yake ya Stargal
Hii Inaenda kuwa EP ya kwanza kwa mtu mzima Spice Diana tangu aanze safari yake ya muziki miaka saba iliyopita