
Staa wa muziki kutoka Uganda, Spice Diana, ameweka wazi msimamo wake kuhusu wimbi la wasanii na wanawake wengi kugeukia upasuaji wa urembo au butt lift ili kubadilisha maumbile yao.
Msanii huyo ambaye anafanya poa na single yake iitwayo “Award” amesema kuwa sababu kubwa inayomzuia ni hofu ya maumivu, akieleza kwamba hataki kitu chochote kinachoweza kuumiza mwili wake.
Licha ya msimamo wake binafsi, mrembo huyo amesisitiza kuwa kila mtu ana uhuru wa kufanya maamuzi kuhusu mwili wake. Anaamini kuwa dunia ya sasa inaruhusu watu kuamua wanachotaka kufanya, iwe ni upasuaji, butt lift au mabadiliko mengine ya kimaumbile, na kwamba haifai mtu yeyote kulaumiwa au kukosolewa kwa uamuzi huo.
Kauli ya Spice Diana inakuja wakati mjadala kuhusu upasuaji wa urembo unaendelea kushika kasi barani Afrika, huku baadhi wakiona ni njia ya kujiamini na wengine wakihofia madhara ya kiafya pamoja na viwango visivyo halisi vya urembo.