
Msanii kutoka nchini Uganda Spice Diana amefunguka sababu kutupiana maneno makali na walinzi alipokuwa jukwaani akitumbuiza katika uwanja wa Bugembe huko Jinja.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni mrembo huyo amesema alikerwa na kitendo cha walinzi kuwazuia mashabiki zake kumkaribia licha kuwa walikuwa wamelipa kiingilio cha shillingi elfu 5 kila mmoja.
Hitmaker huyo wa “Boss” amesisitiza kuwa ataendelea kuwapigania mashabiki zake wamkaribie akiwa anatoa burudani kwenye majukwaa mbali mbali kwa kuwa wao ndio matajiri wake ambao wamekuwa wakifadhili baadhi ya michongo yake.
Hata hivyo vyombo vya usalama vimehoji kuwa hawakutaka kuhatarisha usalama wa mwanamuziki huyo wa Source Management akiwa jukwaani kwa kuwa hawana imani na baadhi ya mashabiki ambao kwa mujibu wao wanaweza kumdhalalisha kijinsia.