Entertainment

SPICE DIANA AKANUSHA BIFU LAKE NA MSANII MWENZAKE AZAWI

SPICE DIANA AKANUSHA BIFU LAKE NA MSANII MWENZAKE AZAWI

Nyota wa muziki kutoka nchini Uganda Spice Diana kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu suala la kuwa kwenye ugomvi na msanii mwenzake Azawi ambaye juzi kati ameshinda tuzo ya Janzi awards mwaka wa 2021.

Hitmaker huyo wa “Upendo” amesema hana ugomvi na Azawi ambaye alishinda tuzo ya msanii bora wa kike kwenye tuzo za  Janzi Awards ila alikuwa anawakosoa waandaji wa tuzo hizo ambao walikuwa wanawatumia vibaya wasanii kwa maslahi yao binafsi.

Spice Diana amesema ana furahia ushindi wa Azawi kwenye tuzo hizo kwani ni moja kati ya wadada ambao wameonyesha uwezo wa kipekee kwenye kazi zake za muziki.

Ikumbukwe Spice Diana hakushinda tuzo hata moja kwenye tuzo za Janzi Awards licha ya kuwa na muendelezo mzuri wa kuachia kazi zake za muziki, jambo lilotafsiriwab na wajuzi wa mambo kuwa mrembo huyo ana machungu ya kutoshinda tuzo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *