Entertainment

Spice Diana Akanusha Taarifa za Kushambuliwa Kuwa Kiki

Spice Diana Akanusha Taarifa za Kushambuliwa Kuwa Kiki

Mwanamuziki kutoka Uganda Spice Diana, amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa tukio la kushambuliwa na wahuni waliokuwa wameabiri boda boda lilikuwa kiki au tukio lililopangwa kwa ajili ya kujitangaza.

Katika taarifa, Spice Diana amesema uvumi kwamba tukio hilo lilipangwa kwa nia ya kujitangaza hauna msingi wowote, akifafanua kuwa wahuni walifuatilia gari lake kwa muda kabla ya kulishambulia.

Mrembo huyo amesema uvamizi huo ulisababisha uharibifu mkubwa kwenye vioo vya nyuma na mlango wa nyuma wa gari. Hata hivyo, Spice Diana amebainisha kuwa yeye pamoja na marafiki zake waliokuwa ndani ya gari walinusurika bila majeraha.

Spice Diana, ametoa shukrani kwa mashabiki wake kwa kumjali na kufuatilia hali yake, lakini akatoa wito kwa umma kutoamini wala kusambaza uvumi au taarifa za uongo kuhusu tukio hilo, akisisitiza kuwa taarifa rasmi zitatolewa kupitia akaunti zake zilizothibitishwa pekee.

Tukio la Spice Diana kushambuliwa na wahuni liliripotiwa kutokea usiku wa Oktoba 17, wakati msanii huyo alipokuwa akirejea nyumbani eneo la Makindye baada ya sherehe za kabla ya siku yake ya kuzaliwa Akiwa njiani kupitia barabara ya Munyonyo, watu wasiojulikana waliokuwa kwenye boda boda walirusha mawe kwenye gari lake, na kusababisha vioo vya nyuma kuvunjika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *