Msanii nyota wa muziki kutoka Uganda, Spice Diana, ameripotiwa kuvishwa pete ya uchumba kwa siri nchini Uingereza.
Taarifa hizo zimechochewa zaidi na mfululizo wa picha na video zilizosambaa mitandaoni zikionyesha mrembo huyo akiwa na pete mpya linaloonekana kama la uchumba.
Katika picha hizo, Spice Diana anaonekana mwenye furaha kubwa huku akiwa kwenye mazingira yanayodaiwa kuwa ya sherehe ya faragha. Hata hivyo, hadi sasa haijabainika ni nani hasa aliyemvisha pete, jambo ambalo limeibua maswali na kuongeza uvumi mtandaoni.
Kwa muda mrefu, Spice Diana amekuwa akihusishwa kimapenzi na aliyekuwa meneja wake, Roger Lubega, ingawa hakuna uthibitisho wowote uliowahi kutolewa kuhusu uhusiano huo.