Entertainment

SPICE DIANA KUACHIA EP YAKE MPYA WIKI IJAYO

SPICE DIANA KUACHIA EP YAKE MPYA WIKI IJAYO

Staa wa muziki kutoka Uganda Spice Diana ameweka wazi tarehe ambayo EP yake mpya ya Star Gal itaingia sokoni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Spice Diana amethibitisha kwamba Ep yake itaingia sokoni Mei 26 mwaka huu baada ya kukamilka kwa hafla ya usikilizaji wa Stargal EP ambayo pia itafanyika siku hiyo.

Licha kuweka wazi tarehe ambayo ataachia EP yake Spice diana hajatuambia idadi ya ngoma pamoja na wasanii aliowashirikisha kwenye Stargal EP ila ni jambo la kusubiriwa.

Stargal EP inaenda kuwa kazi ya kwanza kwa mtu mzima Spice Diana tangu aanze safari yake ya muziki miaka saba iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *