Tech news

SPOTIFY KUWEKA UWEZO WA KUWA-BLOCK WATU

SPOTIFY KUWEKA UWEZO WA KUWA-BLOCK WATU

App ya Spotify kwa mara ya kwanza itaweka sehemu ya ku-block marafiki na watumiaji wa kawaida ambao sio wasanii. Spotify ilikuwa haijaweka sehemu ya ku-block mtu asiweze kuona unasikiliza nini au kufuata akaunti yako. Zamani ilikuwa kama unataka ku-block mtu, inakubidi uwasiliane na wahudumu wa wateja.

Ilichukua muda sana kwa Spofity kuweka uwezo wa ku-block wasanii, tangu mwaka 2014 watu walikuwa wanaomba feature hiyo lakini iliwekwa mwaka 2019 lakini ilikuwa ni ku-block wasanii tu.

Sehemu mpya ya ku-block marafiki itawekwa katika Profile ya mtu unayetaka ku-block, chagua sehemu ya option na utaona option ya ku-block mtu. Feature hiyo itaanza hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *