Msanii wa muziki kutoka Kenya, Stevo Simple Boy, amefunguka tusiyoyajua kuhusu maisha yake kwa kudai kuwa aliwahi kupewa ofa ya kujiunga na kundi la Freemason kwa ahadi ya kulipwa shilingi milioni 10, lakini alikataa.
Akizungumza na Dkt. Ofweneke, Stevo amesema kuwa kulikuwa na kipindi katika safari yake ya muziki ambapo watu wasiojulikana walimshawishi ajiunge na kundi hilo kwa madai ya kumsaidia kupenya zaidi katika tasnia ya muziki. Hata hivyo, msanii huyo amesema alisusia ofa hiyo kwa msimamo wake binafsi na imani alizonazo.
Katika hatua nyingine, Stevo Simple Boy amedai kuwa kuna baadhi ya wasanii katika tasnia ya muziki wanaotumia ushirikina ili kupata umaarufu na mafanikio ya haraka. Kwa mujibu msanii huyo, vitendo hivyo vimechangia baadhi ya wasanii waliofanya poa kipindi cha nyuma kupotea kabisa kwenye muziki.