
Msanii Stevo Simple Boy amenyosha maelezo kuhusu umiliki wa gari aina ya Nissan March aliloinunua hivi karibuni. Hii ni baada ya walimwengu kutilia shaka uhalali wake na kuhoji kwamba msanii huyo amekuwa akitumia magari kutafuta kiki mtandaoni ilhali sio mmiliki halisi.
Kupitia Insta Story yake, Stevo amekanusha kutumia magari kutafuta umaarufu, akisisitiza kuwa safari yake ya maisha inachukua mwelekeo mpya. Amewataka mashabiki waamini maendeleo yake kwani ununuzi wa gari hilo ni sehemu ya mafanikio anayojivunia licha ya changamoto nyingi alizopitia.
Wiki hii, mjadala uliibuka mitandaoni baada ya Stevo kutangaza umiliki wa gari jipya, mashabiki wakibaki na maswali kuhusu ni magari mangapi anamiliki.
Wengine walidai kuwa Nissan March ni gari lake la tatu, wakikumbusha mahojiano ya awali ambapo msanii huyo alikiri baadhi ya magari aliyopiga picha nayo yalikuwa ya kutumia kwa clout pekee.