
Hitmaker wa “Freshi Barida”, Msanii Stevo Simple Boy ameweka wazi kuwa kwa sasa hana mpenzi na anafurahia maisha yake mapya
Msanii wa huyo wa Men in Business ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amefungua milango kwa waliokuwa wanamumezea mate kujaribu bahati yao.
“Mapenzi ya siku hizi jamani, sasa niko single naenjoy. Jamani kua single raha, akinipenda baba na mama inatosha, lakini ata mnivunje roho na mbavu, nikipata mwingine napenda tena”, Ameandika.
Kauli ya Stevo Simple Boy imekuja siku chache baada ya kuvunjika kwa mahusiano yake na mchumba wake Gee, mahusiano ambayo yalidumu kwa kipindi cha miezi sita.