Others

Stevo Simple Boy amfuta kazi meneja wake kwa tuhuma za wizi na usaliti

Stevo Simple Boy amfuta kazi meneja wake kwa tuhuma za wizi na usaliti

Msanii Stevo Simple Boy amemtimua meneja wake mmoja kwenye uongozi wake wa Men In Business baada ya sakata la kukosa kutumbuiza kwenye shoo ya SolFire Fiesta huko Mombasa.

Kupitia video aliyoposti Instagram amesema amechukua hatua hiyo kutokana na usaliti wa meneja ambaye anadaiwa alishirikiana na wandaji kumtapeli pesa zake.

Hata hivyo amewahakikisha mashabiki zake kuwa kila kitu kipo shwari kati yake na mameneja wake wawili waliosalia, hivyo watarajie mambo mazuri kutoka kwake mwakani.

Kauli yake imekuja mara baada ya uongozi wake kupuzilia mbali madai ya Mchekeshaji Eric Omondi kuwa walishinda kumkingia kifua Stevo alipwe pesa zake kabla ya kutumbuiza kwenye tamasha la SolFire Fiesta.

Kwenye mkao na waandishi wa habari uongozi wake ulisema madai ya Omondi hayana ukweli wowote, wakimtaja kuwa msaliti kutokana na kitendo chake cha kuwashinikiza wamruhusu Stevo atokee kwenye shoo kabla ya malipo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *