
Msanii Stevo Simple Boy amepuzilia mbali mahari ya shillingi millioni 2 ambayo mpenzi wake wa zamani Pritty Vishy aliweka wazi kwa wanaume wanaotaka kumchumbia.
Katika mahojiano na mpasho Stevo amesema mrembo huyo anatumia suala kutafuta mazingira ya kuzungumziwa kwenye mitandao ya kijamii kwani dhamani yake haiendani na kiwango cha mahari alichodai.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Freshi Barida” ameweka wazi sababu zilizompelekea kuachana na Vishy kwa kusema kwamba mrembo huyo alimsaliti kimapenzi kwa kutoka kimapenzi na wanaume wengine.
Hata hivyo amekanusha madai ya Pritty Vishy kuwa amekuwa akimlilia warudiane kwa kusema kwamba penzi lao lilivunja kitambo na hawezi kumrudia kutokana na tabia zake ambazo hazikumfurahisha hata kidogo.
Mbali na hayo msanii huyo ambaye chini ya lebo ya muziki ya Men in Business amedokeza ujio wa tamasha lake la Freshi Barida ambalo linalenga kukuza vipaji vya vijana chini.