Entertainment

STEVO SIMPLE BOY APATA HAKIMILIKI YA NEMBO YAKE YA FRESHI BARIDA

STEVO SIMPLE BOY APATA HAKIMILIKI YA NEMBO YAKE YA FRESHI BARIDA

Mwanamuziki Stevo Simple Boy ameripotiwa kusajili jina lake la biashara ambalo ni Freshi Barida.

Taarifa hiyo imethibitishwa na lebo ya muziki ya Men In Business kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram ikisema kuwa Stevo kwa sasa ndiye mmiliki halisi wa jina la Freshi Barida kwa mujibu wa sheria ikizingatiwa tayari amepewa hakimiliki za jina hilo na Ofisi ya Patent ya Kenya.

Lebo hiyo ambayo inasimamia kazi za Stevo Simple Boy imetoa angalizo kwa atakayetumia nembo hiyo bila ridhaa ya msanii huyo na uongozi wake kwa ajili ya shughuli za kibiashara atachukulia hatua kali za kisheria ambayo itajumuisha kulipa faini.

Hii taarifa njema kwa Stevo Simple Boy ambaye juzi kati alizindua bidhaa zake za mavazi za Freshi Barida, siku kadhaa tangu atangaze ujio wa kinywaji chake kiitwacho Freshi Barida Energy Drink.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *