Gossip

Stevo Simple Boy na Mpenzi Wake Brenda Watangaza Wanatarajia Mtoto wa Kiume

Stevo Simple Boy na Mpenzi Wake Brenda Watangaza Wanatarajia Mtoto wa Kiume

Msanii Stevo Simple Boy na mchumba wake Brenda, wameweka wazi kuwa wanatarajia baraka mpya maishani mwao baada ya kutangaza kuwa wanangoja mtoto wa kiume.

Wapenzi hao walifichua habari hizo katika sherehe ya kifahari ya gender reveal iliyofanyika jana, ambapo marafiki na familia walihudhuria kushuhudia tukio hilo la furaha.

Tukio hilo lilipambwa na rangi za buluu na pinki, lakini ilipofika wakati wa tangazo rasmi, rangi ya buluu iliibuka ikithibitisha kuwa wanatarajia mtoto wa kiume.

Sherehe hiyo imepokelewa kwa shangwe na mashabiki wa Stevo Simple Boy mitandaoni, wengi wakimpongeza kwa hatua hiyo kubwa ya kimaisha na kumtakia heri katika safari yake mpya ya kuwa mzazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *