
Inaonekana Msanii Stevo The Simple anataka kugeuza muziki wake kuwa biashara mara baada ya kutangaza ujio wa kinywaji chake kiitwacho ”Freshi Barida”
Msanii huyo amethibitisha taarifa hiyo njema kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram kwa kuachia mashabiki zake swali kama watauunga mkono atakapoingiza bidhaa hizo sokoni.
Stevo the Simple ni moja ya wasanii chipukizi katika tasnia ya muziki nchini Kenya jitihada zake na uwezo wake umekuwa ukionekana kupitia kazi mbalimbali anazozifanya, kama msanii anayechipukia, hii ni moja ya hatua kubwa katika muziki.
Utakumbuka Stevo ambaye yupo chini ya lebo ya muziki ya Men in business amekuwa akitangaza ujio wa ngoma yake mpya ambayo kwa mujibu wake itaingia sokoni Aprili 28 mwaka huu.