
Msanii Stivo Simple Boy kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu tuhuma za kumuibia rapa Rapdon mpenzi wake.
Katika mahojiano yake ameonyosha maelezo kuhusu na madai hayo kwa kusema kwamba madai hayo hayana ukweli wowote na yameibuliwa rapa huyo kwa ajili ya kujitengenezea mazingira ya kuzungumzia kwenye mitandao ya kijamii.
Hitmaker huyo wa “Freshi Barida” amesema uhusiano wake na mpenzi wake ni wa kweli na sio kiki kama namna watu wanavyochukulia mitandaoni.
Sanjari na hilo mpenzi wa Stivo amepuzilia mbali madai ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na rapa don kwa kusema walikuwa marafiki kipindi cha nyuma ila hajawahi toka kimapenzi.
Kauli yao imekuja mara baada ya rapa Rapdon kujitokeza wazi wazi na kudai kuwa Stivo Simple Boy alimvunjia heshima kwa hatua ya kumunyanganya mpenzi wake.