
Msanii wa lebo ya muziki ya Men in Business Stivo Simple Boy ameweka wazi kuachia remix ya smash hit yake iitwayo “Freshi Barida”. Wimbo ambao bado unaendelea kufanya vizuri kupitia majukwaa mbalimbali ya ku-stream muziki mtandaoni.
Stivo Simple Boy ametangaza uwepo wa remix hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amedokeza mpango wa kumshirikisha Mejja, Exray na mkali wa muziki wa Amapiano Ntoshi Gazi kutoka Afrika Kusini kwenye remix ya wimbo wa Freshi Barida.
Kulingana na Meneja wa Stivo aitwaye Vaga, wimbo huo utaingia sokoni juma lijalo na tayari mchakato wa kutayarisha video umeanza huku wasanii walioshirikishwa wakitarajiwa kuhusika kikamilifu kwenye maandalizi ya project hiyo.
Video ya Wimbo wa Freshi Barida ina zaidi ya views laki saba kwenye mtandao wa youtube tangu iachiwe rasmi mwezi mmoja uliopita.