Entertainment

STIVO SIMPLE MBIONI KUJA NA FRESHI BARIDA ENERGY DRINK

STIVO SIMPLE MBIONI KUJA NA FRESHI BARIDA ENERGY DRINK

Msanii Stivo Simple Boy amedokeza mpango wa kuja na kinywaji chake laini (soft drinks) kiitwacho Freshi Barida.

Kupitia ukurasa hitmaker huyo wa Glory amesema kinywaji chake hicho itaingia sokoni au itapatikana kwenye maduka yote nchini hivi karibuni kama mipango yake itaenda vizuri.

“ Na mungu akituzidia zitakua madukani Ivi karibuni tukue freshi barida’” Ameandika Instagram

Utakumbuka Stevo, pamoja na uongozi wake mapema mwaka huu walizindua chapa ya mavazi iitwayo Freshi Barida na tangu ujio wake imepokelewa kwa ukubwa na mashabiki  ambao wamekuwa wamekuwa wakimsapoti Stivo kwa kununua mavazi hayo.

Neno Freshi Barida imekuwa maarufu miomgoni mwa wakenya  na ni jina ya wimbo wa msanii huyo ambao unazidi kufanya vizuri youtube ikiwa na Zaidi ya watazamaji laki 8 huku remix yake ikiwa na watazamaji laki 4.5 ndani ya wiki moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *