Entertainment

Susumila aachia rasmi EP yake mpya

Susumila aachia rasmi EP yake mpya

Mwanamuziki kutoka Pwani ya Kenya Susumila ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Lost Files.

EP hiyo ina jumla ya ngoma saba za moto huku ikiwa kollabo 6 kutoka kwa wakali kama Jollie, Totti, Jacky Chant, Mejja, Jay Crack na Mr. Bado.

Lost Files EP ambayo inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mtandao wa kukisikiliza na kupakua muziki wa Boomplay Kenya ina ngoma kama Mambo, Kiuno, Tetereka, Switi, Niache Niende,na Pweza.

Utakumbuka mara ya mwisho Susumila kutubariki na kazi mpya ilikuwa ni mwaka wa 2021 alipoachia King is King EP iliyokuwa na jumla ya nyimbo 4 za moto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *