
Mwanamuziki mkongwe nchini Susumila ametangaza ujio wa EP yake mpya aliyoipa jina la Lost Files.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema EP hiyo ni mkusanyiko wa nyimbo alizozifanya miaka kadhaa nyuma ambazo kwa njia moja au nyingine hakufanikiwa kuziachia kwa sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake.
Aidha Msanii huyo kutoka 001 Music amesema amechukua hatua ya kuachia EP hiyo kwa ajili ya kupisha njia ya kutoa kazi zake mpya kwa mwaka 2023.
βLost Files Ep ni kazi ambazo nimezifanya kwa miaka kadhaa ambazo kwa sababu moja ama nyingine hazikutoka now kabla nianze kutoa projects ambazo nimeanza kuzifanya huu mwaka nimeamua kuziachia ili tuanze upya tukisonga mbele links ndio hizo zinakuja polepole na shukran in advance Happy New Year…β, Aliandika.
Hata hivyo hajaweka wazi idadi ya ngoma zinazopatikana kwenye Lost Files EP wala wasanii aliowashirikisha ila ni jambo la kusubiriwa.
Utakumbuka mara ya mwisho Susumila kutubariki na kazi mpya ilikuwa ni mwaka wa 2021 alipoachia King is King EP iliyokuwa na jumla ya nyimbo 4 za moto.