
Msanii wa kundi la Ethic Entertainment Swat Matire amefunguka sababu za ukimya wa kundi hilo kimuziki.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Swat amesema mzozo uliobuka kati yao na lebo waliosaini mkataba wakusimamia kazi zao za muziki imesambaratisha juhudi yao ya kuachia kazi kama kundi.
Swat amesema mkataba wao na lebo ulikamilika mwezi Aprili mwaka huu ila kwa sasa wapo mbioni kuhakikisha wanatoa nyimbo walizoahidi kuachia chini ya lebo hiyo ili wawe huru kuendelea na shughuli zao za kimuziki.
Hata hivyo amedokeza ujio wa EP yake mpya ambayo itaingia sokoni mwaka huu lakini pia amewataka mashabiki wakae mkao wa kula kupokea album mpya kutoka kwa kundi la Ethic Entertainment ambayo tayari imekamilika kwa asilimia 100.
Kwa sasa Swat Matire anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Ex aliomshirikisha Shakina Caren.